Mbunge wa Kalangala nchini Uganda afariki akifanyiwa upasuaji

Dismas Otuke
1 Min Read

Mbunge wa eneo bunge la Kalangala nchini Uganda  Hellen Nakimuli,amefariki Jumapili jioni akifanyiwa upasuaji hospitalini.

Kifo cha mbunge huyo wa upinzani kilitangazwa na kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi Jumapili jioni kupitia mtandao wake wa X.

Kifo cha Nakimuli kimetokea chini ya mwezi mmoja kabla ya kuapishwa kwa wabunge hafla itakayoandaliwa kati ya Mei 12 na 13  mwaka huu kufuatia uchaguzi wa Januari 15.

Mbunge huyo alikuwa akifanyiwa upasuaji ambao ulifeli katika hospitali ya Mulago, ingawa  haijabainika ugonjwa aliokuwa akiugua.

Spika wa bunge la Uganda Anita Among ni mmoja wa viongozi waliotoa risala za rambirambi kwa familia ya marehemu ambaye pia alikuwa mchezaji Voliboli.

 

Share This Article