Ruto: Serikali imelainisha operesheni katika sekta ya elimu

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto akutana na viongozi wa mashinani kutoka kaunti ya Marsabit katika Ikulu ya Nairobi.

Serikali imeimarisha sekta ya elimu na kushughulikia changamoto ambazo zimekabili sekta hiyo kwa muda mrefu, amesema Rais William Ruto.

Kiongozi wa taifa alidokeza kuwa serikali imetekeleza mikakati muhimu ambayo imebadilisha sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 23,000, kuwaajiri walimu 100,000 katika muda wa miaka mitatu na kulainisha ufadili wa elimu ya juu.

Alidokeza kuwa serikali imejitolea kuondoa vizingiti vinavyohujumu utoaji wa elimu ya ubora wa hali ya juu, ili kila mwanafunzi apate fursa sawa ya elimu.

Akiwahutubia wajumbe kutoka kaunti ya Marsabit katika Ikulu ya Nairobi siku ya Ijumaa, Rais alidokeza kuwa sekta ya elimu itapokea shilingi bilioni 784.5 kwenye bajeti ya mwaka 2026/2027 iliyowasilishwa bungeni na  John Mbadi.

Kulingana na Ruto, fedha hizo zinalenga kuimarisha masomo na utoaji mafunzo,ili kupiga jeki mageuzi ya kitafa ya nchi hii.

Share This Article