Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC), imetuzwa kwa kutekeleza jukumu kuu katika ukusanyaji wa mapato.
EACC ilikabidhiwa cheti kutoka Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru nchini (KRA),kwa kuwezesha taifa kupata mapato hususan kwa kutwaa mali ya umma ambayo ilikuwa imeporwa.
Huku akimkabidhi Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC Abdi Mohamud cheti hicho, Kamishna wa KRA Mohammed Abdul Mmaka, alisema tuzo hiyo inaashiria umuhimu wa uadilifu na uwajibikaji katika kuimarisha ukusanyaji mapato na kupiga jeki maendeleo ya kitaifa.
EACC ilitambuliwa kwa juhudi hizo za kupigiwa mfano wakati wa mkutano wa wadau wa Halmashauri ya KRA, iliyoandaliwa Aprili 10, 2026 katika Mbuga ya Taifa ya Nairobi.