Rais William Ruto leo Ijumaa anatarajiwa kuhudhuria tamasha za kitaifa za 65 za muziki baina ya shule za upili katika Ikulu ya Nairobi.
Wanafunzi waliotia fora katika mashindano ya muziki,nyimbo na maigizo kwa kawaida huonyesha ueledi wao wanapoalikwa Ikuluni.
Hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wengine,walimu pamoja na maafisa kutoka Wizara ya elimu.