Kaunti ya Bungoma imenufaika na mtambo wa kisasa wa CT scan, unaotarajiwa kupiga jeki utoaji hudfuma za afya kwenye hospitali ya rufaa.
Mtambo huo ulizinduliwa rasmi na Waziri wa Afya Aden Duale siku ya Alhamisi akiambatana na naibu Gavana wa kaunti hiyo Janepher Mbatiany.
Mashine hiyo ilinunuliwa kupitia mpango wa kitaifa wa ununuzi mashine (NESP), kupitia kwa ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Bungoma.