Shujaa kufungua Hong Kong Sevens leo dhidi ya Australia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande- Shujaa,itafungua mkondo wa kwanza wa Hong Kong wa mashindano ya kufuzu kwa msururu wa dunia dhidi ya Australia leo Ijumaa.

Kenya itakabiliana na Australia kuanzia saa sita na dakika 56, katika mechi hiyo ya kundi C,kabla ya kumenyana na New Zealand saa tisa na dakika 47 leo alasiri.

Vijana wa Kevin Wambua watafunga ratiba ya mechi za makundi dhidi ya Marekani kesho saa mbili na dakika 24.

Kenya ilifuzu kwa mashindano ya dunia baada ya kupandishwa ngazi kutoka divisheni ya pili.

Kulingana na mfumo mpya timu 12 ikiwemo Kenya,zitashiriki mikondo mitatu ya Hong Kong mwezi huu na Valladolid nchini Uhispania mwezi  Mei, kabla ya  kumalizia Bordeaux nchini Ufaransa mwezi ujao.

Timu nana bora baada ya mikondo hiyo mitatu zitafuzu kwa mashindano ya msururu duniani mwaka ujao, huku zile zitakazokosa kupenya zikishushwa ngazi.

 

Share This Article