Serikali yatia bidii kufanikisha usawa na ujumuishaji wa kijamii

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki katika mkutano kwenye Jumba la Harambee.

Naibu Rais  Profesa Kithure Kindiki amesema usawa na ujumuishaji wa kijamii  ni matamanio muhimu kwa taifa hili.

Akizungumza afisini mwake katika Jumba la Harambee House Annex, Naibu huyo Rais alisema juhudi zinaendelea zinazonuiwa kuafikia kanuni ya uwakilishi wa kijinsia ya thuluthi mbili.

Aidha, alikariri kuwa, serikali inaimarisha juhudi dhidi ya dhuluma za kijinsia yakiwemo mauaji ya wanawake  na itakuwa inaweka mikakati katika juhudi za kulinda jamii ya wachache pamoja na makundi yaliyowachwa nyuma kimaendeleo.

Prof Kindiki alikariri kuwa ujumuishaji wa makundi maalum kama vile akina mama, watoto, vijana , watu wenye mahitaji maalum, wakongwe, na makundi maalum wanaweza kusaidia katika kuafikia utekelezaji wa masuala muhimu humu nchini.

Naibu Rais aliyasema hayo alipokutana na makamishna wa tume ya kitaifa ya jinsia na usawa-NGEC.

Share This Article