Mabingwa mara nne wa Afrika, Black Stars ya Ghana, wamepatwa na pigo baada ya kiungo wao Thomas Partey, kupigwa breki kuingia nchini Canada kwa Kombe la Dunia.
Hatua hii ina maana kuwa kiungo huyo wa zamani wa Arsenal, atakosa mechi ya ufunguzi ya kundi L, dhidi ya Panama.
Partey ambaye amekuwa kwenye kambi ya Ghana ya Washington DC,nchini Marekani, amenyimwa viza ya kuingia Canada kwa mechi yao ya Jumatano ijayo Juni 17 dhidi ya Panama.
Kiungo huyo Wa Villarreal, alishtakiwa kwa makosa matano ya ubakaji Julai mwaka 2015, nchini Uingereza
Ghana itachuana an Uingereza Juni 23, katika mechi ya pili kabla ya kufungua ratiba ya kundi L dhidi ya Croatia siku nne baadaye