Tshisekedi akubali mazungumzo ya maridhiano

Joto la kisiasa limepanda nchini DRC, kufuatia hatua ya Rais Tshisekedi ,kutangaza kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu mwaka 2028.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Felix Tshisekedi, hatimaye amekubali kufanya mazungumzo ya maridhiano kufuatia shinikizo kutoka kwa viongozi wa kidini ,viongozi wa upinzani na Rais mstaafu Joseph Kabila.

Tshisekedi ameitikia wito huo baada ya kukutana na viongozi wa kidini Julai 17 .

Hatua hiyo imetajwa na wadadisi wa kisiasa kuwa mwanzo mwema katika harakati za kumaliza migogoro ya kiusalama ambayo imekuwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki kwa muda mrefu.

Joto la kisiasa limepanda nchini DRC, kufuatia hatua ya Rais Tshisekedi ,kutangaza kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu mwaka 2028.

Share This Article