Bei ya mafuta aina ya petroli imeshuka kwa shilingi 29 huku dizeli ikipanda kwa shilingi 85 kwa lita moja jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Kulingana na bei mpya iliyotangazwa jana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), petroli itauzwa kwa shilingi 4,086 sawa na shilingi za Kenya 201.31, kutoka bei ya awali ya shilingi 4,115 sawia na shilingi za Kenya 202.74.
Dizeli itauzwa kwa shilingi 4,333 sawa na shilingi za Kenya 213.48 kutoka 4,248 sawa na shilingi za Kenya 209.29 kwa kila lita moja.
Bei hizo mpya zitatumika kati ya Juni 3 na Julai 3.