Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa huenda akasaia mamlakani hadi mwaka 2030 badala ya mwaka 2028, endapo mswada wa kubadilisha katiba ya nchini humo utapitishwa bungeni.
Mswada huo mpya pia unalenga kuondoa muda wa kuhudumu kwa Rais na kumwepusha kupigiwa kura moja kwa moja na raia badala yake atakuwa akichaguliwa na wabunge.
Endapo mswada huo utapita, uchaguzi mkuu wa mwaka 2028 utaahirishwa kumaanisha kuwa Mnangagwa aliye na umri wa miaka 83, atasalia madarakani hadi mwaka 2030.
Mswada huo uliwasilishwa bungeni Jumanne na Waziri wa Sheria Ziyambi Ziyambi, na tayari umeibua hisia kali kuhusu utawala wa Mnangagwa ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 2017.