Magari ya usafiri wa umma kwa mwendo mrefu yakiwemo mabasi ,daladala, magari ya kuagiza mtandaoni na pikipiki, yametangaza bei mpya ya nauli kufuatia kuongezeka kwa bei ya mafuta.
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa ardhini nchini Tanzania (LATRA),ilitoa bei mpya za nauli ambazo zitaanza kutekelezwa baada siku 14 kwa mjibu wa sheria.
Nauli hizo zimepangwa kwa kuzingatia hali ya magari na umbali wa safari.
Mabasi ya kawaida yatalipilisha shilingi 57 za Tanzania sawa na shilingi 2 na senti 80 za Kenya kwa kila kilomita moja kwenye barabara ya lami na shilingi 66.62 sawa na shilingi 3 na senti 31 za Kenya, kwa kilomita moja kwenye barabaraba ya vumbi.
Magari ya kifahari yatalipisha shilingu 74 sawa na shilingi 3 na senti 68 za Kenya kwa kilomita moja ya barabara ya lami.
Pia mabasi ya mijini yaani daladala yatalipisha shilingi 700 za Tanzania sawa na shilingi 34 za Kenya kwa safari ya umbali wa kilomita 10 na shilingi 1500 za Tanzania sawa na shilingi 75 za Kenya kwa safari ya umbali kati ya kilomiya 36 hadi 40.