Bingwa wa Jumuia ya Madola katika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala ,alisajili muda wa kasi mwaka huu alipotimka mbio za Ethiopian Grand Prox kwa sekunde 9.98, mjini Adis Ababa Jumamosi jioni.
Omanyala alitumia mashindano hayo kujiandaa kutetea taji yake nchini Scotland baadaye mwaka huu katika mashindano ya Jumuia ya Madola.
Mwanariadha huyo atakimbia mashindano ya Kip Keino Classic Ijumaa ya Aprili 24.