Rais Ruto afunga safari kuelekea Italia

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Kenya William Ruto amefunga safari ya kuelekea Rome,nchini Italia Jumapili adhuhuri, kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Naibu wake Kithure Kindiki na kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung’wah, walikuwa miongoni mwa viongozi wakuu serikalini waliofika katika angatua ya JKIA kumuaga Rais.

Rais atakutana na Rais wa Italia Sergio Mettarella  na Waziri Mkuu Giorgia Meloni.

Akiwa Italia Rais anatarajiwa kusaini makubaliano ya ushirikiano ya sekta mbalimbali kati ya Kenya na Italia.

Share This Article