Bingwa mtetezi wa mbio za magari nchini WRC Safari rally Kenya, Kalle Rovanperra ataongoza timu ya magari ya Toyota Gazoo katika mashindano yatakayoandaliwa kati ya tarehe 20 na 23 mwezi ujao.
Rovanperra atashirikiana na wenzake kutoka kampuni ya Toyota Elfyn Evans, Katsuta Takamoto, na Sami Pajari kwa makala 73 ya safari rally.
Akizungumza leo wakati wa kuzindua ufadhili wa shilingi milioni 60, Waziri wa michezo Salim Mvurya, amekariri kujitolea kwa serikali kukuza vipaji vya madereva humu nchini.
Afisa Mkuu mtendaji wa WRC Safari Rally
Charles Gacheru amesema matayarisho yamekamilika.
Kampuni ya CFAO imefadhili mashindano ya mwaka huu kwa kima cha shilingi milioni 60.
Mashindano ya Kenya yatakuwa ya mzunguko wa tatu baada ya Monaco na Sweden.