Pipeline yaikomoa VC la Loi, mashindano ya Afrika

Dismas Otuke
0 Min Read

Klabu ya Kenya Pipeline ilisajili ushindi wa tatu,katika mashindano ya ubingwa wa Afrika yanayoendelea jijini Cairo Misri baada ya kuizabua VC la Eloi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo seti 3-0 jana .

Pipeline walipata ushindi wa 25-12,25-12 na 25-17.

Awali Jumanne KPC waliibwaga Gender Light Club kutoka Burundi seti zizo hizo 3-0.

Kenya pia inawakilishwa na KCB na DCI katika mashindano hayo.

TAGGED:
Share This Article