Miamba Arsenal na  Munich wafuzu  nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya

Dismas Otuke
1 Min Read

Ratiba ya mechi za nusu fainali kuwania Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya imebainika kufuatia kukamilika kwa mechi za robo fainali Jumatano usiku.

Arsenal ilifuzu kwa nusu fainali kwa mara ya pili kwa mpigo baada ya kutoka sare tasa na Sportong Lisbon ya Ureno, katika marudio ya kwota fainali ugani Emirates, huku timu hiyo ya Uingereza ikiingia nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa goli moja kwa nunge.

Upande wao Bayern Munich walitoka nyuma mara mbili na kuwakomoa Real Madrid mabao 4-3 ,huku Wajerumani wakiingia nne bora kwa ushindi wa jumla wa magoli 6-4.

Arsenal imeratibiwa kukabiliana na Atletioco Madrid katika nusu fainali wakati Munich ikiwa na miadi dhidi ya mabingwa watetezi PSG katika nusu fainali nyingine.

Munich wataanzia ugenini Ufaransa dhidi ya PSG,April 28 huku The Gunners wakianzia Uhispania tarehe 29 dhidi ya Atletico.

Marudio yatachezwa wiki moja baadaye huku washindi wakifuzu kwa fainali ikipigwa Mei 30 mjini Budapest,Hungary.

Share This Article