Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande ya wanawake ukipenda Kenya Lionesses ilinyakua taji ya kwanza ya kimataifa baada ya kuibuka mabingwa wa mkondo wa kwanza wa mashindano ya Challenger mwaka huu.
Lionesses walitwaa taji hiyo baada ya kuwashinda Argentina alama 17-12 kwenye fainali ya mashindano hayo yaliyoandaliwa nchini Afrika Kusini.
Vipusa wa Kenya walifungua mashindano hayo kw aushindi wa alama 20-5 dhidi ya Samoa ,kabla ya kuilemea Polanda 29-7 na kufuzu kwa nusu fainali.
Kenya iliibwaga Afrika Kusini alama 19-15 katika nusu fainali.