Kenya kushiriki fani 5 pekee Olimpiki ya wasio na uwezo wa kusikia

Buckley Fedha
1 Min Read

Kenya itashiriki katika fani tano pekee kwenye michezo ya Olimpiki kwa wanamichezo wasiokuwa na uwezo wa kusikia baada ya fani saba nyingine kuachwa nje ya kikosi kitakachosafiri.

Kenya ilitarajiwa kushiriki fani 12 lakini sasa fani hizo zimepunguzwa na kusalia tano; riadha, uogeleaji, mpira wa kikapu kwa kinadada, mpira wa mikono kwa wanaume na gofu.

Fani za voliboli ya kinadada, soka ya kinadada, uendeshaji baiskeli, tenisi, tenisi ya mezani, badminton na bowling zimeondolewa kwa sababu ya ukosefu wa fedha.

Wachezaji kwenye timu hizo zilizoachwa nje watarejeshewa pesa walizotumia huku taifa hili likitarajia kuwakilishwa na jumla ya wanamichezo 177.

Michezo hiyo itaandaliwa baina ya tarehe 15 na 26 mwezi  ujao.

Buckley Fedha
+ posts
Share This Article