Maafisa wawili wa Polisi wakamatwa kwa madai ya kupokea rushwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Afisa wa cheo cha juu wa polisi akamatwa kwa madai ya kupokea hongo.

Tume ya Maadili na Vita dhidi ya Ufisadi (EACC), imewakamata Maafisa wawili Wakuu wa Polisi kwa madai ya kuitisha hongo kutoka kwa wananchi.

Wawili hao walikamatwa baada ya malalamishi kuwasilishwa kuwa Afisa Mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kaunti ndogo ya Kitutu ya Kati Inspekta Mkuu Nicholas Waringa, pamoja na Corporal Lovy Ochieng Ouya wa kituo cha polisi cha  Nyanchwa  wameitisha hongo ya shilingi 100,000 ili kumkamata mshukiwa anayedaiwa kujenga kwenye ardhi ambayo sio yake.

Maafisa wa EACC walianzisha uchunguzi dhidi ya maafisa hao wawili na kuwakamata baada ya kupokea shilingi 40,000 kutoka kwa mlalamishi.

“Washukiwa hao walipelekwa katika afisi kuu za EACC inayosimamia kanda ya Kisii, ambako waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 50,000 kila mmoja, wakisubiri kukamilika kwa uchunguzi,” ilisema taarifa ya EACC kupitia ukurasa wa X.

EACC ilielezea kujitolea kwake kukabiliana na ufisadi, ikito wito kwa Wakenya kuendelea kuripoti visa vya utoaji rushwa na utumizi mbaya wa mamlaka.

TAGGED:
Share This Article