Moto wazuka kwenye bweni Hill School, wanafunzi wanusurika

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya KRCS

Wanafunzi wapatao 340 wa kidato cha 3 na 4 walinusurika baada ya moto kuzuka kwenye shule ya upili ya Hill School, Eldoret leo Jumanne alfajiri. 

Moto huo, uliozuka majira ya saa kumi na moja, umedhibitiwa.

Shirika la Msalaba Mwekundu, KRCS, linasema hakuna majeruhi walioripotiwa kwani wanafunzi wote walikuwa darasani moto huo ulipozuka.

KRCS inasema inafanya kazi kwa karibu na mratibu wa kaunti ya Uasin Gishu, polisi, zima moto na jamii ya eneo hilo kurejesha hali ya kawaida.

Wanafunzi walioathirika wanapatiwa ushauri wa kisaikolojia wakati kiwango cha uharibifu kikikadiriwa.

 

Share This Article