Rais William Ruto amefannya kikao na bilionea wa Nigeria Aliko Dangote, kuhusu kiwanda cha kusafisha mafuta katika eneo la Lamu.
Ruto na Dangote walikutana mjini New York Marekani pembezoni mwa kongamao la Umoja wa mataifa (UNGA).
Mazungumzo hayo yalihusu ufadhili wa mradi huo ambao utapanua fursa za kawi ya Kenya na ukanda wote kwa jumla ,kubuni nafasi za ajira na kuongeza thamani.
Pindi kiwanda hicho kitakapokamilika kitapanua uwezo wa Afrika Mashariki katika usambazaji mafuta na kuwainua kichumi wakazi wa eneo hili.
Rais yuko Marekani kuhudhuria Kongamano la 81 la Umoja wa mataifa litakaloanza kesho.