FIFA World Cup: Uswizi waiduwaza Canada mbele ya halaiki

Ushindi huo ulihakikisha Uswizi wanaongoza kundi B kwa pointi 7, wakifuatwa na Canada kwa alama 4.

Dismas Otuke
1 Min Read

Uswizi iliongoza kundi B la fainali za Kombe la Dunia baada ya kuwazima wenyeji Canada mabao 2-1 katika mchuano wa mwisho wa kundi hilo jana usiku katika uchanjaa wa BC mjini Vancouver Jumatano usiku.

Juan Vargas na Johan Manzambi walipachika magoli ya Uswizi kunako dakika 46 na 57 mtawalia, naye David Promise akawafungia wenyeji goli la kufutia machozi.

Ushindi huo ulihakikisha Uswizi wanaongoza kundi B kwa pointi 7, wakifuatwa na Canada kwa alama 4.

Bosnia Hezgovina ilichukua nafasi ya tatu kwa pointi 4 pia, baada ya kuwalabua Qatar mabao 3-1 katika mechi nyingine ya mwisho ya kundi hilo iliyochezwa sambamba mjini Seattle.

Qatar iliyaaga mashindano baada ya kumaliza ya mwisho kwa alama moja pekee.

Share This Article