Nairobi na Pwani zatarajia mvua kubwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Maeneo ya Nairobi na Pwani ya Kenya yanatarajia mvua kubwa kati ya Jumatatu, Aprili 27, na Mei 4.

Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini imetoa tahadhari kwa Wakenya wanaoishi maeneo hayo.

Pia mvua kubwa inatarajiwa katika nyanda za juu na Magharibi mwa Bonde la Ufa na kaskazini mashariki.

Maeneo hayo pia huenda yakakumbwa na mafuriko kutokana na mvua hiyo kubwa.

Aidha, Wakenya wame tahadharishwa dhidi ya kuendesha magari na pikipiki au kutembea ndani ya maji ya mafuriko.

Kaimu Mkurugenzi wa idara hiyo Edward Muriuki,amesema mvua ya milimita 20, inatarajiwa nchini kati ya Jumatatu usiku Na Jumanne Aprili 28,katika maeneo mengi nchini .

 

 

Share This Article