Iran imeishutumu Marekani kwa kuweka matakwa kupindukia kuwa sababu kuu iliyochangia kutibuka kwa mazungumzo ya kumaliza vita.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Abbas Araghchi amesema haya Jumatatu alipokutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Rais wa Marekani Donald Trump alifutilia mbali safari ya wajumbe wakuu wa serikali yake nchini Pakistan wiki jana, akisema endapo Iran inataka mazungumzo, itahitaji kwenda Marekani au kuwapigia simu.
Mvutano kuhusu mlango wa bahari wa Strait of Hormuz umesambaratisha mazungumzo.