Serikali ya Afrika Kusini imewatuma wataalam jijini Paris kuchunguza chanzo cha kifo cha Balozi wake nchini Ufaransa, Nathi Mthethwa.
Mwili wa Nathi, aliye na umri wa miaka 58, ulipatikana chini ya hoteli ya Hyatt Regency baada ya kuripotiwa kuanguka kutoka orofa ya 22 mapema mwezi huu.
Maafisa watano wa polisi kutoka Afrika Kusini watashirikiana na wataalam wa Ufaransa kubaini kilicho sababisha kifo hicho.
Inaaminika kuwa Nathi aliacha barua akiomba radhi kwa kujitoa uhai, kuashiria kuwa alijiua kwa kujirusha chini.