Mwanamke wa umri wa miaka 45, amekamatwa na polisi Jumamosi, kuhusiana na kifo cha Daktari wa afya ya uzazi Job Obwaka .
Polisi wamesema mwanamke huyo alikuwa mtu wa mwisho kuonekana na marehemu kabla ya kukimbizwa katika hospitali ya Nairobi, alipotangazwa kufariki Ijumaa Mei Mosi.
Yamkini marehemu alisafiri hadi Kitengala Ijumaa, walipokutana na mwanamke huyo na kula kula chakula cha mchana pamoja kabla ya mkutano wao wa kibiashara.
Dkt Obwaka, aliripotiwa kuanguka na kuzirai akiwa Kitengela, kabla ya kukimbizwa katika hospitali ya Nairobi, aliporipotiwa kufariki punde alipowasilishwa saa moja usiku.
Mwanamke huyo amezuiliwa katika kituo cha Polisi cha Kilimani, kusaidia kwa uchunguzi.