Waamuzi kutoka Mor0cco wameteuliwa kusimamia derby ya Kariakoo, kati ya Simba na Yanga, kuwania alama za ligi kuu tanzania bara kati ya Simba na Yanga, siku ya Jumapili, katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kisiwani Zanzibar.
Refa wa kati atakuwa Hamza El Faruq akisaidiwa na msaidizi wa kwanza Lahsene Azkawi,na Hamza El Nasri, atakayekuwa msaidizi wa pili huku Mostafa Kchaaf, akiwa afisa wa nne
Derby hiyo Kariakoo itachezwa siku nne tu, baada ya Simba kuwashinda Yanga bao moja kwa bila kwenye mchuano wa fainali ya kombe la Muungano.
Wekundu wa Msimbazi Simba, watahitaji ushindi ili kukata uongozi wa Yanga hadi alama 2, wakati Yanga maarufu kama Jangwani Boys, wakilenga ushindi ili kutanua uongozi wao hadi 8, kileleni pa jedwali.
Yanga wanashikili kukutu uongozi wa Ligi hiyo kwa pointi 47, wakifuatwa na Simba kwa alama 42,alama 5 zaidi ya Azam United FC, wanaokalia nafasi ya tatu.
Tiketi za mzunguko ni zinauzwa kwa shilingi 15,000 za Tanzania sawia na shilingi 743, za Kenya.
Vingilio kwa tiketi za VIP B ni shilingi 30,000, za Tanzania, ukipenda shilingi 1,500 za Kenya, na 50,000 za Tanzania au shilingi 2,500 za Kenya, kwa tiketi za VIP A.