CHAN 2024:Tanzania yataja kikosi

Taifa Stars watafungua kampeni yao ya kundi B, dhidi ya Burkina Faso Agosti 2, katika uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkapa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tanzania imetaja kikosi cha makala ya nane ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani almaarufu CHAN.

Kikosi hicho cha kocha Hemed Suleiman kinawajumuisha wachezaji wengi wa vilabu vya Simba na Yanga ambavyo vimekuwa na msimu wa kufana.

Simba waliocheza hadi fainali ya kombe shirikisho wametoa wachezaji sita sawia na Azam FC huku mabingwa wa Ligi Kuu Yanga wakichangia wanandinga wanne.

Taifa Stars watafungua kampeni yao ya kundi B, dhidi ya Burkina Faso Agosti 2, katika uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkapa.

Timu nyingine katika kundi hilo ni pamoja na Mauritania, Madagascar na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 

Website |  + posts
Share This Article