Mechi za makundi kufuzu AFCON mwaka 2027, kuanza Septemba

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF), limetangaza kuwa mechi za makundi kufuzu kwa kipute cha kombe la AFCON mwaka ujao zitaanza Septemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa CAF mechi mbili za kwanza hatua ya makundi zitachezwa Septemba 21 na Oktoba 6 mwaka huu.

Mechi za raundi ya pili na tatu zitaandaliwa kati ya Novemba 9 na 17 mwaka huu, nazo zile za mzunguko wa tano na sita zichezwe baina ya Machi 22 na 30 mwaka ujao.

Jumla ya mataifa 48 yatashiriki mechi hizo za makundi 12 za kufuzu AFCON, ambapo timu 2 bora kutoka kila kundi, zitajikatia tiketi zikijumjiusha wenyeji Kenya,Tanzania na Uganda.

Fainali za 36 za AFCON zitafanyika kati ya Juni 19 na Julai 17 mwaka ujao. .

Share This Article