Mtangazaji wa soka Diblo Kaberia afariki

Kaberia alikuwa mwanachama wa chama cha waandishi wa habari za michezo nchini Kenya (SJAK).

Dismas Otuke
0 Min Read

Mtangazaji nguli wa soka Diblo Kaberia ameaga dunia mapema siku ya Jumapili baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Hadi kifo chake, Kaberia alikuwa mtangazaji soka katika idhaa ya Radio Jambo kwa zaidi ya miaka 10.

Marehemu alikuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Ruaraka Uhai Neema, kaunti ya Nairobi na alikuwa afanyiwe upasuaji.

Kaberia alikuwa mwanachama wa chama cha waandishi wa habari za michezo nchini Kenya (SJAK).

Share This Article