Harambee Stars kuzipiga dhidi ya Lesotho leo

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars itashuka mjini Pretoria, Afrika Kusini kupimana ubabe na Lesotho katika mchuano wa pili wa kujipima nguvu.

Kenya na Lesotho zitachuana katika pambano hilo la kuanzia saa kumi alasiri, baada ya kwenda sare ya bao moja katika mchuano wa kwanza Juni 4.

Kenya inatumia mechi hizo kunoa makali kwa mechi za kuanzia Septemba za kufuzu fainali za AFCON mwaka ujao.

Share This Article