Gor Mahia washinda ubingwa wa Ligi Kuu Kenya, baada ya APS kuwafyatua Chui

Ni mara ya kwanza kwa K'ogalo kunyakua ubingwa tangu msimu wa mwaka 2023/2024 kabla ya kupoteza taji msimu uliofuatia kwa Police FC.

Dismas Otuke
1 Min Read

Gor Mahia siku ya Jumapili walitawazwa mabingwa wa Ligi Kuu Kenya kwa mara ya 22 bila kugusa mpira baada ya wapinzani wao wa karibu AFC Leopards kushindwa kumakinika mchezoni.

Leopards wameikabidhi Gor kombe baada ya kupoteza mabao 2-1 ugenini Bomet dhidi ya APS.

Gor ambao mchuano wao wa ugenini dhidi ya Mara Sugar katika uwanja wa Raila Odinga kaunti ya Homa Bay, ulisimamishwa na mahakama, wanaongoza jedwali kwa 68 huku wakisalia na mechi mbili.

Leopards wanakalia nafasi ya pili kwa alama 64 wakibakisha mechi moja.

Ni mara ya kwanza kwa K’ogalo kunyakua ubingwa tangu msimu wa mwaka 2023/2024 kabla ya kupoteza taji msimu uliofuatia kwa Police FC.

Gor Mahia wameshinda ligi miaka ya 1968, 1974, 1976, 1979, 1983, 1984, 1985, 1987, 1990, 1991, 1993, 1995, 2013, 2014, 2015, 2017, 2018, 2018–19, 2019–20, 2022–23, 2023–24 na 2025/2026.

Sirkal sasa watawakilisha Kenya katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Share This Article