Mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia ya nusu marathon Joyceline Jepkosgei, ameibuka mshindi wa makala ya mwaka huu ya mbio za nusu marathoni za Barcelona zilizoandaliwa Jumapili nchini Uhispania./strong>
Jepkosgei, ambaye ni bingwa wa London mwaka 2021, ameziparakasa mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 1 dakika 4 na sekunde 13.
Alexandra García Jadraque wa Uhispania alimaliza wa pili kwa saa 1 dakika 5 na sekunde 28, huku Gladys Chepkurui wa Kenya akinyakua nishani ya shaba kwa saa 1 dakika 6 na sekunde 25.
Mbio za wanaume zilishindwa na Mganda Jacob Kiplimo.