Timu ya Jamaica inayowajumuisha Ackeem Blake, Tina Clayton, Kadrian Goldson na Tia Clayton, imeandikisha rekodi mpya ya dunia ya mbio za mita 100 kwa wanariadha wanne mseto katika mbio za Dunia zilizoanza Jumamosi nchini Botswana.
Jamaica imezikamilisha mbio hizo katika mchujo wa tatu, wakitwaa ushindi kwa muda wa sekunde 39.99, wakiboresha rekodi ya sekunde 40.07, iliyokuwa imewekwa na Canada katika mchujo wa kwanza .
Mbio hizo za Dunia kupokezana kijiti zinatumika kuwania tiketi kwa mashindano ya Riadha ya Dunia mwaka ujao mjini Beijing,Uchina, hali kadhalika mashindano ya Ultimate Septemba mwaka huu mjini Budapest Hungary.