Rais wa Shirikisho la kandanda nchini Kenya,FKF,Hussein Mohammed amepuuzilia mbali hatua ya baraza kuu kupiga kura ya kumtimua afisini siku ya Ijumaa, akisisitiza kuwa angali kinara na kamwe hatetereki.
Akizungumza Jumamosi na wanahabari, Hussein amesema mkutano ulioandaliwa na baraza kuu NEC haikufuata utaratibu ufaao na kamwe hakujuzwa.
Kuhusu zabuni ya shilingi milioni 42 iliyozua ubishi,Hussein amekanusha kuwa FKF, ililipa kampuni hiyo ya bima na kuweka bayana kuwa malipo hayo yalifanywa na shirikisho la soka barani Afrika kulingana na desturi za maandaliazi ya mashindano.
Aidha,amesema yuko tayari kufanyiwa uchunguzi kuhusiana na tuhuma za ufisadi.
Yamkini sakata hiyo ilitokea mwaka jana wakati wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika CHAN.