Serikali imetangaza kupunguza bei ya miwa inayowasilishwa na wakulima viwandani kwa shilingi 250 kwa kila tani moja kote nchini.
Halmashauri ya sukari nchini ilitangaza kuwa tani moja ya miwa itakuwa ikinunuliwa kwa shilingi 5,500, kutoka bei ya awali ya shilingi 5,750 kwa tani moja.
Bei hiyo mpya iliafikiwa na kamati ya muda ya kuweka bei kwa kuzingatia gharama ya uzalishaji,bei ya soko katika ukanda wa Afrika Mashariki na mapendekezo ya wadau.
Pia kupunguzwa kwa bei ya miwa kumechochewa na kupungua kwa bei ya sukari kwa gunia la kilo 50 kutoka shilingi 7,000 hadi kati ya shilingi 6,000 na shilingi 6,100 kwa sasa.
Bei ya tani moja ya miwa nchini Tanzania ni shilingi 4,900,ilihali nchini Uganda tani moja inanuliwa kwa shilingi 4,500 za Kenya.