Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan mapema Jumamosi amezindua meli ya kwanza ya uvuvi wa bahari kuu.
Hafla ilifanyika katika makao makuu ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Kigamboni Jijini Dar es Salaam .
Meli hiyo itafanikisha shughuli za uvuvi nchini humo ambayo ni mojawapo wa vitega uchumi wa nchi.