Serikali kutumia shilingi bilioni 54 kwa miradi ya maendeleo Baringo

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure kindiki akagua miradi ya maendeleo Baringo.

Serikali itatumia shilingi bilioni 32 kwa ujenzi wa kilomita 854 za barabara, ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, masoko ya kisasa, mabweni na nyumba za taasisi mbali mbali katika kaunti ya Baringo.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, alisema mradi wa uunganishaji stima kwa nyumba 4,000 zaidi unatekelezwa kwa kitita cha shilingi milioni 712, huku ujenzi wa Taasisi ya mafunzo kuhusu mifugo ya Mogotio ukiendelea kwa kima cha shilingi milioni 200.

Kindiki alisema usambazaji stima katika sehemu za mashambani, umepiga jeki hali ya maisha ya wakazi na kufanikisha ukuaji wa biashara ndogo ndogo.

Aliyasema hayo siku ya Ijumaa alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo katika eneo bunge la Motio, kaunti ya Baringo.

Wengine walioandamana naye ni pamoja na Naibu Gavana wa Baringo County Felix Kipng’ok, Seneta Vincent Chemitei, wabunge, wawakilishi wadi na viongozi wa mashinani.

Share This Article