Ongezeko kubwa la mafuta siyo tu humu nchini bali duniani kote limetokana na mzozo unaoendelea kwa sasa Mashariki ya Kati ukihusisha nchi za Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Hata hivyo, Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki anasema serikali imedhamiria kuwakinga Wakenya dhidi ya athari za mzozo huo.
“Ushuru ziada wa thamani wa VAT umepunguzwa kutoka 16%, bilioni 12 tayari zimetumiwa kutoa ruzuku kwa bei za mafuta katika kipindi cha miezi miwili iliyopita na ruzuku zaidi zitatolewa kwa akiba zijazo hadi hali ya kawaida irejee,” amesema Kindiki.
“Kuanzia leo, bei ya dizeli imepunguzwa kwa shilingi 10 kwa lita kama ishara ya serikali kuendelea kushirikiana na wadau kufikia usimamizi endelevu wa ongezeko la bei ya mafuta duniani.”
Naibu Rais amesema ushuru uliodumishwa ni muhimu kwa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara ili kuunga mkono ujenzi wa uchumi nchini.