Ruto aanza ziara ya siku mbili nchini Kazakhstan

Nchi hizo mbili zimekuwa zikikuza uhusiano mzuri kwa miongo kadhaa kupitia mfululizo wa ushirikiano wa kimakusudi.

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto amewasili nchini Kazakhstan kwa ziara ya siku mbili. 

Nchi hizo mbili zimekuwa zikikuza uhusiano mzuri kwa miongo kadhaa kupitia mfululizo wa ushirikiano wa kimakusudi.

Ruto anasema wakati umewadia wa kuboresha uhusiano huo hata zaidi.

Kenya na Kazakhstan hushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo huku ushirikiano katika biashara ya maua, mbolea, na usafirishaji ukinawiri kati ya nchi hizo mbili.

“Kenya imejitolea kujenga kwa msingi huu kwa kutumia fursa mpya katika fedha, iCT, utalii, nishati na mipango ya mabadilishano, huku lengo kuu likiwa kubuni nafasi za ajira, uhamishaji wa ujuzi, na pia kupanua na kufungua masoko mapya ya bidhaa zetu,” alisema Ruto.

Share This Article