Msivamie Mahakama ya Upeo, LSK yahimizwa

Tom Mathinji
2 Min Read
LSK yahimizwa kutovamia Mahakama ya upeo.

Idara ya Mahakama imeelezea wasiwasi wake kuhusu taarifa ya Chama cha Wanasheria hapa nchini, LSK iliyotolewa Januari 23,2025, iliyowahimiza wanachama wake kuandamana hadi Mahakama ya Upeo kufuatia uamuzi wa mahakama hiyo kumpiga marufuku mwanasheria Ahmednasir Abdullahi pamoja na kampuni yake ya sheria na washirika.

Kupitia kwa taarifa iliyotolewa na msemaji ya Idara ya Mahakama Paul Ndemo siku ya Jumatatu, kesi kuhusu kumpigwa marufuku kwa wakili huyo, kwa sasa inashughulikiwa katika mahakama kadhaa, ikiwemo Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu.

Kulingana na idara hiyo, kesi hizo ni pamoja na:

  • Kesi kati ya Chama cha wanasheria nchini na Mahakama ya Upeno ya Kenya na Abdullahi SC na wengine 19. Katika Mahakama Kuu
  • Kesi kati ya Ahmednasir Abdullahi na Jaju Mkuu Martha Karambu Koome na wengine tisa.
  • Kesi kati ya Ahmednasir Maalim Abdullahi na Mwanasheria Mkuu. Katika Mahakama ya Afrika Mashariki kuhusu haki.
  • Kesi kati ya Mahakama ya Upeo ya Kenya na LSK. katika Mahakama ya Upeo.

Idara ya Mahakama ilisema kesi hizo zote bado hazijakamilika na zingali mikononi mwa mahakama na kwamba hazipaswi kujadiliwa kwa umma.

Aidha idara hiyo ya mahakama imetoa wito kwa wanachama wa LSK, kufuata sheria na kuheshimu hatua ya kutojadili kesi zinazoendelea mahakamani hadharani.

“Tunatoa wito kwa LSK kutochukua hatua hiyo. Tunawahimiza kuzingatia sheria kutatua swala hilo,” ilisema taarifa ya LSK.

Website |  + posts
Share This Article