Wanafunzi kadhaa wanahofiwa kufariki kwenye mkasa wa moto ulioteketeza bweni la Shule ya Wasichana ya Sekondari ya Juu ya Utumishi Girls Academy mjini Gilgil, kaunti ya Nakuru mapema leo Alhamisi.
Yamkini moto huo ulizuka majira ya saa tisa unusu alfajiri, wakati wanafunzi walikuwa wamelala kwenye bweni.
Wengi wa wanafunzi walishindwa kujinusuru baada ya milango ya bweni kukataa kufunguka.
Shirika la Msalaba Mwekundu, KRC, limetenga kituo cha kuwasaidia majeruhi na kutoa ushauri nasaha.
Wanafunzi wengine kadhaa waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika Hospitali ya St. Joseph.
Chanzo cha moto huo bado hakijulikani huku uchunguzi ukiendeshwa na maafisa wa polisi.