Morocco ndilo taifa bora barani Afrika katika viwanda, kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Maendeleo barani Afrika (AfDB) ya mwaka 2025.
Ripoti hiyo ilitolewa pembezoni mwa mkutano mkuu wa kila mwaka wa AfDB wa mwaka 2026 mjini Brazaville nchini Congo.
AFB ilizindua ripoti ya uorodheshaji wa mataifa ya Afrika kuhusu ustawi wa kiviwanda (AII) Pamoja na ripoti ya Africa Industrial Investment Barometer (AfIIB).

Aidha, kulingana na ripoti hiyo, ukuaji wa viwanda barani Afrika ungali chini huku biashara baina ya mataifa ya Afrika ukiwa asilimia 14.4 ya biashara zote barani humo.
Ripoti hiyo inaelezea kuwa mataifa 41 kati ya 54 ya Afrika yaliongeza uwezo wao wa kiviwandani.
Morocco imeipiku Afrika Kusini kama taifa lenye uchumi thabiti barani Afrika kutokana na kuimarika kiviwanda.