Mashabiki wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Marekani, kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola.
Hatua hiyo imelazimu shirikisho la kandanda DRC(FECOFA), kutaka mashabiki hao warejeshewe pesa za tiketi walizokuwa wamenunua.
Chui wa Congo wamefuzu kwa Kombe la Dunia mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974.
Marekani imepiga marufuku raia wa kutoka mataifa ya DRC,Sudan Kusini au Uganda na wasio Waamerika na waliokuwa DRC kwa wiki tatu zilizopita, kuingia nchini Marekani, kama tahadhari ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola.
DRC imerekodi visa zaidi ya 900 vya Ebola na vifo vipatavyo 223, huku shirika la Afya Ulimwenguni (WHO ),ikitangaza ugonjwa huo kuwa tishio na wala sio janga.