IEBC yaidhinisha 9 kugombea kiti cha ubunge cha Ol Kalou

Uchaguzi huo mdogo utaandaliwa Julai 16 mwaka huu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wawaniaji tisa kutoka vyama tofauti wameidhinishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kuwania ubunge wa Ol Kalou katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kuandaliwa mwezi Julai mwaka huu.

Tisa hao ni Abdulahi Abdifatah Hussein wa chama cha Federal Kenya,Timothy Kamau wa chama cha People’s Renaissance, Samuel Muchina wa United Democratic Alliance, na Edward Mathenge kutoka chama cha Kenya Moja Movement.

Wengine ni Rachael Wangui wa chama cha People’s Democratic Party, Wilson Kigwa wa Jubilee, Stephen Wanyoike wa chama cha National Liberal, Kamau Ngotho wa Democray for Citizens na Edwin Muchiri wa PNU.

Kiti hicho kilibaki wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo hilo David Kiaraho.

Uchaguzi huo mdogo utaandaliwa Julai 16 mwaka huu.

Share This Article