Mudavadi: China imepiga jeki maendeleo ya miundombinu ya Kenya

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi na balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi amesema Kenya na China zitaendelea kuimarisha ushirikiano wao wa muda mrefu uliojikita kwenye malengo ya maendeleo ya pamoja.

Kwenye mkutano na balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, alisema walijadili kubuni mbinu za kupanua ushirikiano huo chini wa mkakati thabiti kati ya nchi hizo mbili.

“China imepiga jeki maendeleo ya miundombinu ya Kenya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, barabara ya Nairobi Expressway, barabara Kuu ya Thika, na bandari ya Lamu chini ya mradi wa LAPSSET miongoni mwa miradi mingine.

Aidha, kulingana na Mudavadi, viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu kuboresha ushirikiano katika biashara na uwekezaji, teknolojia, kilimo na uhusiano kati ya watu, huku nchi hizo mbili zikiendelea kufanikisha ukuaji endelevu.

Share This Article