Mwili waopolewa kutoka tanki la maji taka lililoporomoka Mombasa

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwili waopolewa kutoka tanki la maji taka lililoporomoka Mombasa.

Mwili umeopolewa kutoka kwa tanki la maji taka lililoporomoka siku ya Jumapili kaunti ya Mombasa.

Watu wawili walizama ndani ya tanki hilo la maji taka, lilipoporomoka wakati watu walipokuwa wakitazama mezi za ligi kuu nchini Uingereza, katika eneo la Bamburi Mwisho, wadi ya Kadzandani, kaunti ndogo ya Nyali jijini Mombasa, .

Mwili wa Abdallah Aziz Abdallah mwenye umri wa miaka 54, uliopolewa saa sita na dakika arobainne na tisa, ukiwa mwili wa kwanza kuopolewa tangu kutokea kwa mkasa huo mwishoni mwa wiki.

Mwili huo ulipelekwa katika hospitali kuu ya Pwani, ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa ukumbi huo unaotumika kuonyesha mechi za ligi kuu Uingereza, umepigwa marufuku kutumika, huku biashara hiyo ikihudumu bila leseni.

Afisa mkuu anayehusika na maswala ya kuzima-moto katika kaunti ya Mombasa Ibrahim Basafar, alisema tanki hilo la maji taka lina kina cha futi 120.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article