Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Morocco,Atlas Lions,Mohamed Ouahbi ametangaza kikosi cha wanandinga 26, watakaoshiriki fainali za Kombe la Dunia kuanzia mwezi ujao.
Kocha Ouabi amewadumisha wengi wa wachezaji waliokuwa katika fainali za mwaka 2022 nchini Qatar, na kombe la AFCON, mwaka uliopita wakiwa wenyeji.
Morocco waliocheza hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022 watafungua dimba kundini C, dhidi ya mabingwa mara tano Brazil,kabla ya kukabiliana na Scotland Juni 20 na hatimaye kucheza na Haiti siku tano baadaye.

Makala ya 23 ya Kombe la Dunia yataandaliwa kwa pamoja na Marekani,Canada na Mexico, kati ya Juni 11 na Julai 19 mwaka huu.