Simba na Yanga kuvaana Dabi ya Kariakoo Jumapili

Dismas Otuke
2 Min Read

Miamba na watani wa jadi Tanzania bara, vlabu vya Simba na Yanga watachuana tena Jumapili hii Mei 3, kwenye mechi ya Ligi kuu NBC.

Derby hiyo Kariakoo itachezwa siku nne tu, baada ya Simba kuwashinda Yanga bao moja kwa bila kwenye mchuano wa fainali ya kombe la Muungano.

Mechi hiyo ambayo ni ya 169, baina ya timu hizo hasimu itasakatwa katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kisiwani Zanzibar.

Wekundu wa Msimbazi Simba, watahitaji ushindi ili kukata uongozi wa Yanga hadi alama 2, wakati Yanga maarufu kama Jangwani Boys, wakilenga ushindi ili kutanua uongozi wao hadi 8, kileleni pa jedwali.

Yanga wanashikili kukutu uongozi wa Ligi hiyo kwa pointi 47, wakifuatwa na Simba kwa alama 42,alama 5 zaidi ya Azam United FC, wanaokalia nafasi ya tatu.

Tiketi za mzunguko ni zinauzwa kwa shilingi 15,000 za Tanzania sawia na shilingi 743, za Kenya.

Vingilio kwa tiketi za VIP B ni shilingi 30,000, za Tanzania, ukipenda shilingi 1,500 za Kenya, na 50,000 za Tanzania au shilingi 2,500 za Kenya, kwa tiketi za VIP A.

Pambano hilo litasimamiwa na mwamuzi kutoka Morocco, wakiongozwa na Refa wa kati Hamza El Faruq.

Wasaidizi wake watakuwa Lahsene Azkawi,na Hamza El Nasri, atakayekuwa msaidizi wa pili huku Mostafa Kchaaf akiwa afisa wa nne.

Share This Article